1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi Zimbabwe

28 Agosti 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, ameyapinga matokeo rasmi ya uchaguzi uliomrejesha madarakani Rais Emmerson Mnangagwa, huku waangalizi wa kimataifa wakisema haukukidhi viwango vya kidemokrasia.

https://p.dw.com/p/4Vdfs
Simbabwes wichtigster Oppositionsführer Nelson Chamisa
Picha: Tsvangirayi Mukwazhi/AP Photo/picture alliance

Chamisa anayeongoza muungano wa upinzani wa Citizens Coalition for Change (CCC) alisema wameshinda uchaguzi huo na wana viongozi, akiongeza kuwa walishangazwa kusikia Mnangagwa akitangazwa mshindi.  

Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC), Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 52.6 akimuangusha mpinzani wake wa karibu, Chamisa, aliyetangazwa kupata asilimia 44.

Soma zaidi: SADC: Uchaguzi Zimbabwe haujakidhi mahitaji ya katiba
Matokeo ya kwanza ya majimbo yatolewa Zimbabwe

Mapema, Mnangagwa aliwataka wanaoyapinga matokeo hayo kwenda mahakamani.

Waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walielezea mashaka yao kwenye mchakato mzima wa uchaguzi huo tangu kwenye kuzuiwa kwa mikutano ya wapinzani, uandikishwaji wa wapiga kura, upendeleo wa vyombo vya habari hadi kutishwa kwa wapigakura.