Urusi inasema ilizuia njama ya kuuwawa afisa na mwanablogu
28 Desemba 2024Matangazo
Shirika hilo ambalo linaendelea kazi ya lile lililokuwepo katika nyakati za lililokuwa Shirikisho la Usovieti, KGB, limesema raia mmoja wa Urusi alifanya mawasiliano kwa Telegramu na afisa wa shirika la kiintelijensia la Ukraine, GUR. FSB haikumtaja afisa au mwanablogu ambao walikuwa wanalengwa na njama hizo. Shirika la Ujasusi wa kijeshi la Ukraine GUR halikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tuhuma hizo. Itakumbukwa mnamo Desemba 17, idara ya ujasusi ya Ukraine, SBU, ilimuua kwa bomu kamanda wa kitengo cha kemikali na kibaolojia cha wanajeshi wa Urusi, Luteni Jenerali Igor Kirillov, mjini Moscow. Kyiv ilikuwa inamshutumu kwa kuendeleza matumizi ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku, jambo ambalo Moscow inalikanusha.