1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa wapya wa kivita

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2024

Urusi na Ukraine zimebadilishana wafungwa wapya wa kivita ambapo kila upande umepokea jumla ya wafungwa 95 katika makubaliano mapya yaliyoratibiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu.

https://p.dw.com/p/4lyjD

Urusi na Ukraine zimebadilishana wafungwa wapya wa kivita ambapo kila upande umepokea jumla ya wafungwa 95 katika makubaliano mapya yaliyoratibiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kulingana na wizara ya ulinzi ya Urusi, wafungwa wa nchi hiyo walioachiwa wanafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu nchini Belarus, mojawapo ya mshirika wa karibu wa Moscow katika vita vya zaidi ya miaka miwili.

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amesema wafungwa wa nchi hiyo waliwahi kuhudumu katika nafasi tofauti kwenye uwanja wa mapambano, ikiwemo katika mji wa bandari wa Mariupol mwaka 2022. Kwa mujibu wa Kamishna wa haki za binadamu wa bunge la Ukraine, mabadilishano hayo ni ya 58 tangu kuanza kwa vita hivyo na kufanya jumla ya wafungwa waliorejea nyumbani kufikia 3,767.