Urusi na Ukraine zashambuliana vikali na droni
11 Novemba 2024Mashambulizi hayo yanafanyika licha ya mazungumzo yanayoripotiwa kufanywa baina ya Rais Vladimir Putin na rais mteule wa Marekani, Donald Trump, ripoti zilizokanushwa na Kremlin.
Soma pia: Trump azungumza na Putin, aonya dhidi ya kusambaa kwa mzozo nchini Ukraine
Mashambulizi ya anga ya Urusi yamewaua watu watano kusini mwa Ukraine, siku moja baada ya Moscow na Kyiv kuanzisha mashambulizi ya droni katika usiku mmoja. Kulingana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, Urusi ilirusha droni zipatazo 145 kuanzia usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, ikiwa ni zaidi ya usiku wowote katika mzozo huo.
Urusi pia nayo imedai kuzidungua ndege 34 zisizo na rubani za Ukraine zilizoilenga Moscow siku ya Jumapili, likiwa ni jaribio kubwa zaidi la kushambulia mji mkuu huo tangu kuanza kwa vita mwaka 2022.