SiasaUkraine
Urusi: Ujerumani inazidi kujiingiza kwenye vita vya Ukraine
2 Mei 2023Matangazo
Kulingana na Moscow, serikali mjini Berlin haina namna yoyote ya kuhakikisha kwamba silaha ilizoipatia Ukraine hazitotumika dhidi ya maeneo ya Urusi.
Hayo yameelezwa na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov ambaye amesema silaha za Ujerumani zilizopelekwa Ukraine tayari zinatumiwa kwenye vita katika eneo la Donbas,ambalo Urusi imeshalitangaza kuwa eneo lake.
Kwa upande mwingine serikali ya Ukraine mjini Kiev imesema Urusi imebadili mbinu katika vita nchini humo na sasa imeanza kuyalenga kwa makusudi maeneo ya makaazi ya watu katika mashambulizi yake ya anga.
Mshauri wa rais Volodymry Zelensky, Mykhailo Podolyak amesema hakuna shaka kwamba Urusi inafanya mashambulizi dhidi ya makaazi ya raia au maeneo yenye makaazi mengi ya raia.