Urusi, Ukraine zaendelea kushambuliana
4 Agosti 2024Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vilikikomboa kijiji hicho kinachopatikana katika eneo la Donetsk ambako vikosi vyake vimekuwa vikifanya mashambulizi.
Katika hatua nyingine, ndege moja isiyo na rubani ya Ukraine imemuuwa mwanamke mmoja katika mji wa Shebekino kwenye eneo la Belgorod nchini Urusi. Taarifa hiyo imethibitishwa Gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov leo Jumapili. Wakati huohuo, maafisa wa Moscow wamesema, Ukraine imeishambulia na kuizamisha manowari ya kivita ya Urusi.
Kulingana na maafisa hao, droni moja ya Ukraine ilishambulia pia jengo lililokuwa na mfumo wa anga kuzuia makombora. Mfumo huo ulikuwa ukitumika kulilinda daraja la Kerch ambalo ni muhimu kwa kusafirishia na kusambaza vifaa muhimu kwa vikosi vya Urusi.