1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaapa kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya Ukraine

26 Novemba 2024

Jeshi la Urusi limeahidi kujibu mashambulizi mapya ya anga yanayofanywa na Ukraine ndani ya Urusi kwa kutumia makombora ya Marekani aina ya ATACMS.

https://p.dw.com/p/4nRo1
Mkoa wa Zaporizhzhia wa Ukraine
Mkoa wa Zaporizhzhia wa UkrainePicha: Dmytro Smolienko/Avalon/Photoshot/picture alliance

Jeshi la Urusi limeahidi kujibu mashambulizi mapya ya anga yanayofanywa na Ukraine ndani ya Urusi kwa kutumia makombora ya Marekani aina ya ATACMS.

Kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema inapanga hatua za kulipiza kisasi bila ya kutoa maelezo zaidi.

Wizara hiyo imeongeza kwamba Ukraine ilifanya mashambulizi mapya kwa kutumia makombora hayo kwa siku mbili wiki iliyopita.

Marekani iliipa Ukraine ruhusa ya kutumia silaha hizo kushambulia eneo la Urusi mapema mwezi huu baada ya miezi kadhaa ya maombi kutoka kwa Kyiv.

Katika hali isiyo ya kawaida, Urusi imekiri kwamba mashambulizi hayo mapya yamesababisha uharibifu wa vifaa vya kijeshi na kuwajeruhi baadhi ya wafanyakazi wake.