Urusi yaishambulia tena Kyiv kwa makombora
7 Februari 2024Matangazo
Kulingana na ujumbe wa meya wa mji wa Kyiv, Vitali Klitschko, katika mtandao wa Telegram, mifumo ya ulinzi wa angani imeharibu baadhi ya makombora hayo.
Haya yanafanyika wakati ambapo mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, akiwa amesafiri kuelekea Ukraine, kutazama hali ilivyo katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya kilichotekwa na Urusi.
Soma zaidi:Ukraine yakataa wito wa Urusi kwa Mariupol kujisalimisha
Akizungumza na waandishi wa habari, Grossi, alisema mfumo wa usambazaji wa maji ya kukipoza kinu hicho uliathirika kufuatia uharibifu uliofanywa katika Bwawa la Kakhovka.