Urusi yakubali kurefusha makubaliano ya ngano
17 Mei 2023Matangazo
Hatua hii ni afueni kwa usalama wa chakula duniani baada ya vita vya Ukraine vilivyoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita kusababisha ongezeko la bei za vyakula.
Urusi ilikuwa imeweka Alhamis (Mei 18) kuwa muda wa mwisho kwa maslahi yake kuzingatiwa la sivyo ijiondoe kutoka kwenye makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa.
Kuongezwa kwa makubaliano hayo ni hatua muhimu kwa nchi za Afrika, Mashariki ya Kati na baadhi ya sehemu za Asia ambazo zinategemea nafaka, mafuta na bidhaa za vyakula vya bei rahisi kutoka Ukraine.