1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Urusi yampongeza Trump kwa kuikosoa Ukraine

13 Desemba 2024

Urusi imempongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump kwa kukosoa hatua ya Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa kutumia makombora ya masafa marefu iliyopewa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4o7aY
Donald Trump na baadhi ya viongozi wa Ulaya wamekuwa wakijadili namna ya kumaliza vita nchini Ukraine.
Donald Trump na baadhi ya viongozi wa Ulaya wamekuwa wakijadili namna ya kumaliza vita nchini Ukraine.Picha: Christophe Petit Tesson/POOL/AFP/Getty Images

Trump amekosoa uamuzi wa Rais Joe Biden wa kuiruhusu Kyiv kutumia makombora hayo na kuuita usio wa busara na ambao haukupaswa kuchukuliwa kwa sababu unavichochea vita hivyo.

Wakati Urusi ikizidisha kasi ya mashambulizi yake, Trump na baadhi ya viongozi wa Ulaya wamekuwa wakijadili namna ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Lakini Ikulu ya Kremlin imesema bado ni mapema mno kuzungumzia wazo la kupeleka wanajeshi wa kulinda amani nchini Ukraine.