1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia vituo vya kijeshi Ukraine

1 Januari 2024

Urusi imesema imeshambulia vituo vya kijeshi katika mji wa Ukraine, Kharkiv na kuharibu majengo za makaazi ya watu, hoteli na vituo vya afya, ikiwa ni kujibu shambulio lililofanywa na Ukraine huko Belgorod.

https://p.dw.com/p/4akfb
Ukraine Charkiw | Zerstörung Palace Hotel nach Raketenangriff
Picha: Vitalii Hnidyi/REUTERS

Msemaji wa katika eneo la Kharkiv amesema, makombora sita yaliyorushwa yamejeruhi watu wasiopungua 28, huku yakifuatiwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.Katika taarifa yake Urusi imesema, shambulio hilo lililoipiga hoteli ya zamani Kharkiv Palace, na makao makuu ya huduma za usalama ya Ukraine limewaua miongoni mwa maafisa wa kijeshi na ujasusi, sambamba na mamluki wa kigeni na wapiganaji waliokua wanajiandaa kufanya uvamizi eneo la mpakani, ambao waliohusika katika shambulio laUkraine dhidi ya Belgorod. Msemaji wa jeshi wa Ukraine Andriy Yusov, ameviambia vyomba vya habari vya ndani kuwa hakuna kitu chochote cha kijeshi kilicholengwa katika shambulio hilo wala mtu wa kada yake aliedhurika.