1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yaushambulia mji wa nyumbani wa Zelensky wa Kryvyi Rih

25 Desemba 2024

Mtu mmoja ameuawa na wengine zaidi ya 12 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la makombora ya Urusi kwenye mji wa kusini-mashariki mwa Ukraine wa Kryvyi Rih.

https://p.dw.com/p/4oYtq
Ukraine | Kryvyj Rih
Jengo la ghorofa lililolengwa kwa shambulio la kombora la Urusi katika mji wa Kryvyi Rih, eneo la Dnipropetrovsk.Picha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Mwanamke mmoja ameokolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi vya nyumba iliyoharibiwa na shambulio hilo la makombora.

Mkuu wa utawala wa jeshi wa eneo hilo, Oleksandr Vilkul, amesema shambulio hilo lilipiga jengo la makaazi katika mji huo uliokuwa na wakaazi 600,000 kabla ya vita.

Soma pia: Makombora ya Urusi yailenga Kyiv na kuua watu karibu 11 

Mkuu wa ofisi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Andriy Yermak, alichapisha nyumba iliyoharibiwa katika mtandao wa Telegram na kuongeza kuwa, kufikia jana jioni, idadi ya majeruhi ilikuwa 15.

Kryvyi Rih, mji wa nyumbani wa Rais Volodymyr Zelensky, umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na makombora na droni.