1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yazidi kuharibu miundombinu ya Ukraine

2 Januari 2023

Baada ya siku tano mfululizo za mashambulizi ya anga kote nchini Ukraine, meya wa mji wa Kiev Vitali Klitschko amesema miundo mbinu ya nishati imeharibiwa vibaya.

https://p.dw.com/p/4Ld9O
Vitali Klitschko
Picha: John Moore/Getty Images

Vitali Klitschko amesema, mashambulizi hayo hayo dhidi ya miundombinu yamesababisha kukatika kwa umeme. Hata hivyo meya huyo ameeleza kuwa usambazaji wa maji haukuathirika.

Klitschko ameongeza kuwa, mvulana wa miaka 19 anapokea matibabu hospitalini baada ya jengo alilokuwemo kushambuliwa.

Ving'ora vya tahadhari vimesikika usiku kucha katika sehemu kubwa ya Ukraine ambayo katika siku za hivi karibuni imeshuhudia mashambulizi makubwa ya Urusi. Wanajeshi wa Urusi wanaripotiwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani za Iran aina ya Kamikaze.

Wanablogu wa kijeshi wa Urusi wameripoti kuwa nchi hiyo imeyalenga maeneo ya Poltava, Kharkiv, Donetsk, Dnipropetrovsk, Mykolaiv, Kherson na Kiev katika wimbi la mashambulizi lililoanza siku ya Alhamisi.