Urusi:Tumedungua drone 5 za Ukraine, hakuna madhara
4 Julai 2023Msemaji wa wizara ya mambo ya nje urusi amesema jaribio la serikali ya Kyiv kushambulia eneo ambalo ni miundombinu ya raia ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege ambapo unapokea ndege za kimataifa, ni kitendo kipya cha kigaidi.
Taarifa za jeshi la Urusizinasema ndege nne zisizokuwa na rubani ziliharibiwa na mifumo ya ulinzi ya anga huku moja kati ya ndege hizo tano ikipunguzwa ukali kwa njia ya kielektroniki kabla ya kuanguka bila kueleta madhara.
Kwa ujibu wa vyombo vya habari vya ndani huduma za dharura zilipelekwa katika maeneo hayo ikiwa takriban kilometa 40 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vnokovo ambapo utendaji kazi ulitatizwa kwa muda.
Soma pia:Urusi,Ukraine washindwa kufikia mwafaka huko Uturuki
Shirika la usafiri wa anga la Urusi limesema safari za ndege nyingi zimehamishiwa katika viwanja vya ndege vingine na msongamano umeshuhudiwa kuanzia majira ya kumi na moja alfajiri kwa saa za Urusi.
Shirika hilo limesema katika viwanja vingine huko mjini Moscow havijaathiriwa na tukio hilo hivyo safari zimeendelea kama kawaida.
Zelensky:Hatuna mifumo thabiti ya ulinzi wa anga
Huko nchini UkraineRais Volodymyr Zelenskiyamesema taifa lake bado halina idadi ya kutosha ya mifumo thabiti ya ulinzi wa anga dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya Urusi.
Zelensky katika hotuba yake ya kila jioni amesema vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi ya anga katika mji wa Sumy wakilenga maeneo ya kiraia ikiwemo majengo ya makaazi ya raia.
"Kwa bahati mbaya, taifa letu bado halina idadi ya kutosha ya mifumo thabiti ya ulinzi wa anga"
Alisema Zelensky na kuongeza kuwa mifumo ya kulinda eneo lote na kuangusha shabaha zote za adui bado si thabiti.
"Adui hutumia fursa hii, kama walivyofanya leo kushambulia kigaidi kwenye mji wa Sumy"
Shambulio la vikosi vya Urusi katika mji huo wakitumia ndege zisizokuwa na rubani za Irani, ililenga, majengo ya makazi na jengo la Huduma ya Usalama ya Ukraine.
Mchakato wa Ukraine kujiunga na NATO
Katika mchakato wa Ukraine kujiunga na NATO rais wa Lithuania Gitanas Nauseda amewataka washirika wa muungano huo kuondoa hofu kwamba kuipa Ukraine uanachama katika muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na Marekani ni kuichokoza Urusi ambayo iliivamia Ukraine mwaka uliopita.
Soma pia:Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg aahidi msaada zaidi kwa jeshi la Ukraine
Amesema badala yake hatua hiyo itaongeza ufanisi kwa Kyiv katika uwanja wa mapambano, kwenye kuvikabili na kuvifurusha vikosi vya Urusi, Ukraine.
Naerais Vladimir Putin leo akihutubia katika mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai amewaambia viongozi wa Iran,China na wengine, kwamba Urusi inapinga na itaendelea kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi kutokana na operesheni kubwa ya kijeshi ya Moscow nchini Ukraine.