Utafiti: Watu milioni 17.5 ni maskini nchini Ujerumani
13 Desemba 2024Matangazo
Hali hiyo imetokana na viwango vya juu vya kodi na gharama zinazohusiana na kodi za nyumba.
Kulingana na data za Ofisi ya Takwimu, kaya nyingi hutumia zaidi ya theluthi moja ya mapato yao kulipia gharama ya makazi, huku baadhi zikitumia zaidi ya nusu ya pato lao.
Hayo yakiarifiwa, mauzo ya nje ya Ujerumani yamepungua kwa asilimia 2.8 mnamo mwezi Oktoba ikilinganishwa na mwezi uliopita, huku uchumi wake ukitarajia kushuhudia ukuaji mdogo mwaka ujao baada ya kushuka kwa asilimia 0.2 mwaka huu.