Tarehe 31 Agosti huadhimishwa siku ya dawa za mitishamba barani Afrika. Nchini Burundi siku hiyo iliyoadhimishwa wiki chache baada ya tarehe hiyo ilikuwa fursa kwa shirika la afya duniani kubaini kuwa matumizi ya dawa za mitishamba Burundi yafikia asilimia 90. Waziri wa afya anasema serikali italeta kifaa kitakachosaidia kupima kiwango cha dawa ya mitishamba kinachohitajika kupewa mgonjwa.