1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki na Armenia zarejesha uhusiano wa kibalozi

Sekione Kitojo11 Oktoba 2009

Umoja wa Ulaya umeikaribisha hatua ya Uturuki na Armenia kuanzisha tena uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/K3r6
Duka katika mtaa mmoja wa Istanbul nchini Uturuki.Picha: AP

GENEVA

Umoja wa Ulaya umeikaribisha hatua ya Uturuki na Armenia kuanzisha tena uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Katika taarifa yake, Umoja wa Ulaya uliitaja hatua hiyo kama ya ujasiri yenye lengo la kuleta amani na udhabiti baina ya majirani hao wawili. Uturuki na Armenia zilitia saini makubaliano hayo jana jioni, mjini Geneva baada ya mzozo wa muda mrefu . Sherehe za kutia saini mkataba huo zilicheleweshwa kwa muda, baada ya tofauti kuibuka, kuhusiana na maandishi ya makubaliano hayo, lakini maafisa wa Marekani akiwemo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton wakasaidia kuleta maafikiano. Makubaliano hayo yanaanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia na kufungua mpaka wa Uturuki na Armenia. Uhusiano kati ya majirani hao wawili ulizorota tangu mauaji ya halaiki ya Warmenia chini ya utawala wa Ottoman mwaka wa 1915. Armenia imeshikilia mauaji hayo ni mauaji dhidi ya binadamu, lakini Uturuki imekana madai hayo. Raia wa Lebanon wenye asili ya Armenia waliandamana mjini Beirut kupinga kutiwa saini kwa makubaliano hayo.