1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaahidi kuimarisha mahusiano na Afrika

4 Novemba 2024

Uturuki imeahidi kuimarisha mahusiano yake na bara la Afrika na kulitolea mwito bara hilo kuunga mkono juhudi za kidiplomasia za serikali mjini Ankara za kuwaunga mkono Wapalestina.

https://p.dw.com/p/4mZSM
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Gokhan Balci/AA/picture alliance

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa ngazi ya mawaziri kati ya Uturuki na mataifa ya Afrika uliofanyika mwishoni mwa juma nchini Djibouti. Nchi 14 za Afrika zilihudhuria mkutano huo, ikiwemo Angola, Chad, Visiwa vya Comoro, Sudan Kusini, Zambia na Zimbabwe. 

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uturuki Hakan Fidan aliyeongoza mkutano huo amesema biashara kati ya Uturuki na Afrika ilipindukia dola bilioni 35 mwaka uliopita na uwekezaji wa nchi yake barani Afrika tayari umefikia thamani ya dola bilioni 7. 

Soma pia: Uturuki kujiunga kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel

Uturuki imeendelea kuwekeza kwa wingi barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni na kiongozi wake Rais  Recep Tayyip Erdogan amefanya ziara 50 kwenye mataifa 31 ya bara hilo katika muda wa miongo miwili ambayo amekuwa madarakani.