Uturuki yafyetua mizinga dhidi ya maeneo ya kaskazini mwa Irak
14 Oktoba 2007Baghdad:
Jeshi la nchi kavu la Uturuki limefyetua mizinga dhidi ya mji wa Nezdour,kaskazini mwa Irak ,umbali wa kilomita tano karibu na mpaka wa Uturuki.Mashahidi wanasema hakuna hasara iliyopatikana.Hujuma hizo zimefuatia mwito wa Marekani na Umoja wa ulaya kuisihi Uturuki ijizuwie.Serikali ya waziri mkuu Racep Tayyeb Erdogan ilionya hapo awali wanajeshi wake wanaweza kuvuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Irak kuwaandama wanamgambo wa kikurd wa chama cha PKK.Viongozi wa Uturuki wamekua wakilalamika, waasi hao wa PKK wanatumia eneo la kaskazini la Irak kufanya mashambulio nchini mwao.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, amesema amewaonya maafisa wa serikali ya Uturuki dhidi ya kuivamia sehemu ya kaskazini mwa Irak ,akihoji uamuzi kama huo utazidi kuviruga utulivu nchini Irak.Maafisa wawili wa ngazi ya juu wa Marekani wako Uturuki kujaribu kuwatuliza viongozi wa serikali ya Ankara.