Uturuki yajitolea upatanishi mzozo wa Urusi na Ukraine
9 Machi 2024Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amerejelea pendekezo lake la kuwakutanisha maafisa wa Ukraine na Urusi kwa mazungumzo ya amani. Erdogan ametoa pendekezo hilo, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Istanbul alipomkaribisha Rais Volodmyr Zelensky wa Ukraine.
Kiongozi huyo wa Uturuki, amesema nchi yake ipo tayari kuandaa mkutano wa kilele wa amani utakaoishirikisha Urusi, na pia kufanya upatanishi ili kumaliza vita kwa amani kwa njia ya mazungumzo. Ukraine inapinga pendekezo la Urusi kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa kimataifa.Zelensky kufanya ziara nchini Uturuki na atakutana na Erdogan
Akizungumza katika mkutano huo, Zelensky alisema Urusi inaweza kushiriki mazungumzo hayo ikiwa itakubaliana na matakwa ya kuwaondoa wanajeshi wake kikamilifu katika ardhi ya Ukraine.
Mazungumzo ya viongozi hao pia yalijikita katika hatua mpya itakayotoa hakikisho la usalama wa meli za kibiashara katika Bahari Nyeusi.