Uturuki yamrejesha nyumbani balozi wake wa Marekani
12 Oktoba 2007Matangazo
Serikali ya Uturuki imemrejesha nyumbani kwa muda balozi wake nchini Marekani.Uamuzi huo umepitishwa kufuatia azimio la kamisheni ya baraza la wawakilishi la Marekani linalozungumzia juu ya mauwaji ya halaiki ya waarmenia milioni moja na nusu, yaliyofanywa na watawala wa enzi ya Ottoman, katika vita vikuu vya kwanza vya dunia.Uturuki iliyochipuka mwaka 1923 toka enzi za Ottoman,ingawa imekiri mauwaji yamefanyika,inapinga lakini kama yalikua mauwaji ya halaiki.waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan amesema anasubiri kuona kura ya baraza la wawakilishi la Marekani itapita vipi,kabla ya kuamua hatua gani zaidi za kuchukua.