1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yashambulia tena waasi.

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfdo

Ankara. Ndege za kijeshi za Uturuki zimeshambulia maeneo ya waasi kaskazini mwa Iraq kwa siku ya pili mfululizo. Afisa wa Kikurd nchini Iraq amesema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kwa muda wa saa tatu lakini hayakusababisha madhara. Kwa zaidi ya wiki, jeshi la Uturuki limefanya operesheni kadha dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi PKK. Serikali ya Uturuki inadai kuwa maelfu ya wapiganaji wa kundi la PKK wanaitumia ardhi ya Iraq kufanya mashambulizi ndani ya Uturuki na kusema kuwa itaendelea kutumia nguvu dhidi ya waasi hao.