1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yatahadharishwa dhidi ya hatua ya kijeshi

11 Oktoba 2007

Waziri mkuu wa Uturuki kufikisha swala la kuchukuliwa hatua za kijeshi waasi wa Kikurdi wa PKK wa kaskazini mwa Irak mbele ya bunge

https://p.dw.com/p/C7iB
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: AP

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa leo kuliomba bunge la nchi hiyo liidhinishe kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Kikurdi huko kaskazini mwa Irak.

Uturuki inaamini kwamba waasi hao wamekuwa wakijificha kwenye eneo hilo.

Marekani imeitahadharisha Uturuki dhidi ya kutuma vikosi vyake vya kijeshi huko kaskazini mwa Irak kuwaandama waasi hao wafuasi wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi cha PKK.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Sean McCormack amesema, kwa matazamo wa nchi yake hatua ya kijeshi ya Uturuki hadi ndani ya Irak haitaleta suluhisho la kudumu.

Wanajeshi 15 wa Uturuki wameuwawa katika mashambulio ya chama cha PKK.