Vettel na Leclerc wagongana na kutolewa katika Grand Prix
18 Novemba 2019
Sebastian Vettel na Charles Leclerc wamekabiliana na shutuma kali kutoka kwa mkuu wa timu ya magari hayo ya Ferrari Mattia Bonotto baada ya magari yao kugongana na kuondolewa katika mashindano ya jana Jumapili ya Grand Prix nchini Brazil. Madereva hao walikuwa wakiwania kumalizika katika nafasi ya nne wakati walipogongana wakati Vettel alilipiza kisasi kwa kupitwa na dereva mwenzake wa Ferrari.
Max Verstappen ameweka alama yake kama bingwa wa hapo baadae jana kwa ushindi kwa magari ya Red Bull katika mbio hizo za Grand Prix nchini Brazil.
Kwa taarifa hiyo ndio sina budi kusema tumefikia mwisho wa habari hizi za michezo jioni ya leo, tutembelee katika ukurasa wetu wa michezo, kwa habari zaidi katika dw.com, michezo, jina langu ni Sekione Kitojo, kwaheri.