1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Vifo kutokana na pombe yenye sumu India vimeongezeka hadi 50

23 Juni 2024

Idadi ya vifo kutokana na aina fulani ya pombe haramu yenye sumu nchini India imeongezeka hadi 53, huku idadi kadhaa ya wa manusura iliyopo hospitalini ikiendelea kuathiriwa zaidi na pombe hizo.

https://p.dw.com/p/4hOnr
Pombe iliyotengenezwa katika mitaa ya Calcutta
Wanaume wa Kihindi wanakunywa pombe katika eneo la kuuzia pombe huko Calcutta, Mashariki mwa India, 23 Oktoba 2013Picha: picture alliance/dpa

Waziri Mkuu wa jimbo la Tamil, Nadu Stalin amesema kinywaji hicho kilichotengenezwa kienyeji kilichanganywa na methanol yenye sumu na kuwauwa watu 37 ndani ya saa chache baada ya kunywa pombe hiyo haramu siku ya Jumanne.

Zaidi ya watu wengine 100 walikimbizwa hospitalini, lakini wengine walikuwa katika hali mbaya sana ambayo sio rahisi kuweza kuokolewa uhai wao.

Mamia ya watu hufa kila mwaka nchini India kutokana na pombe za bei nafuu zinazotengenezwa kwenye viwanda vya kienyeji, lakini tukio hili la sasa ni baya zaidi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.