Vijana wanaambukizana Ukimwi kwa kukosa elimu
29 Oktoba 2013Hali hiyo inatokana na wao kukosa elimu ya uzazi. Kutokana na hatua hiyo, UNESCO imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo kwa nchi kuhaksha kwamba mitaala ya elimu inakidhi viwango vya elimu ya uzazi itayowasaidia vijana hao kufanya maamuzi pindi watapojihusisha na masula ya mapenzi. Hayo yamebainika nchini Tanzania wakati shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilipozindua ripoti mpya kuhusu vijana na balehe yenye kauli mbiu isemayo “Vijana wa Leo-Muda wa kuchukua hatua sasa”
Katika utafiti wake uliofanya katika mataifa 21, yaliyoko Kusini na Mashariki mwa Afrika, UNESCO ilibaini kasoro kadhaa ikiwemo kukosekana kwa mitaala maalumu inayoangazia afya za uzazi kwa vijana. Hali hiyo ndiyo iliyotajwa kuwa imechangia kwa kiwango kikubwa kwa vijana hao kutokuwa na maamuzi sahahi pindi wanapoanza kujishughulisha na masuala ya kipamapenzi.
Utafiti huo pia ambao umewajumuisha wataalamu kutoka taasisi za umma, mashirika ya kiraia nay ale ya Umoja wa Matifa ikiwemo UNICEF na WHO, inanoyesha kuwa, kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi kwa makundi ya vijana kumesabisha mamia ya wanafunzi wa kike kuacha shule kila siku kutokana na kupata mimba.
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mtaalamu wa UNESCO Mathias Faustini alisema kkuwa pamoja na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la mimba shulenni na upunguzwaji maambukizi ya virusi vya HIV kwa vijana, lakini ozeefu umeonyesha kuwa juhudi hizo zimekosa mikakati ya kisanyansi.
Hata hivyo ili kukabiliana na hali hiyo UNESCO kushirikiana na nchi zilizoko katika Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika(Sadc) na zile zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuteleza mpango wa pamoja ambao uhakikisha elimu kwa vijana inaboreshwa.
Tayari mkakati wa awali umeandaliwa ambao utajadiliwa katika kikao kinachotazamiwa kufanyika mwanzoni mwezi Disemba nchini Afrika Kusin, kikiwa husisha mawaziri Wizara za Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Elimu na Masuala ya ufundi kutoka katika nchi zote wanachama.
Baadhi ya makundi ya wanafunzi pamoja na watetezi wa maslahi ya vijana yameanza kupaza sauti yakitoa mwito kwa mamlaka za kidola kuanz akumulika utendaji wake wa mambo.
Kuanzishwa kwa mkakati huo wa upitiaji mitaala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kunatajwa na wengi pengine kunaweza kusaidia kupunguza matatizo yanayowaandama vijana wananza kubalehe.
Mwandishi: George Njogopa
Mhariri: Josephat Charo