Vikosi vya Syria vyaendelea kukabiliana na waasi Aleppo
2 Desemba 2024Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Waziri Mkuu wa Syria.
Syria imewapeleka kwa haraka wanajeshi wa ziada kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika juhudi za kuwarejesha nyuma waasi hao waliofanya mashambulizi ya kushtukiza na ambao sasa wanadhibiti mji wa Aleppo.
Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza wametoa wito wa usitishwaji wa mapigano nchini Syria wakitaka kulindwa kwa raia na miundo mbinu, huku Iran na Urusi zikisema zitaendelea kumuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad na kumsaidia kukabiliana na waasi hao.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ilisema zaidi ya watu 14,000 - karibu nusu wakiwa watoto - wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo.
Mashambulizi hayo yamezuka wakati nyeti kwa Syria na eneo hilo la Mashariki ya Kati. Ikiwa ni siku mbili tu baada ya hatua tete ya usitishaji wa mapigano kati ya kundi la Hezbollah na Israel katika nchi jirani ya Lebanon.