1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ukraine vyafanya operesheni 'iliyofaulu' Dnipro

17 Novemba 2023

Jeshi la wanamaji la Ukraine limesema kwamba vikosi vyake vimefanya misururu ya mashambulizi kwenye ukingo wa mashariki wa mto Dnipro unaokaliwa na Urusi karibu na mji wa kusini wa Kherson.

https://p.dw.com/p/4Z1Zx
Andrij Jermak |  Anayeongoza ofisi ya rais Volodymr Zelenski
Andriy Yermak, Mkuu wa ofisi ya rais wa UkrainePicha: Ruslan Kaniuka/Ukrinform/ABACA/picture alliance

Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mtandao wa kijamii wanajeshi hao wa majini wameongeza kuwa vikosi vyao "vimefanikiwa kupiga hatua mbele katika maeneo kadhaa. 

Mapema wiki hii, Andriy Yermak, mkuu wa ofisi ya rais wa Ukraine, alisema wanajeshi wa Ukraine wanafanya kazi ya "kuwaondoa wanajeshi wa Urusi na zana za kivita" katika rasi ya Crimea na wameshafanikiwa ukubwa wa asilimia 70 katika rasi hiyo.

Zelensky: Usambazaji wa silaha Ukraine umepungua kutokana na vita vya Israel na Hamas

Mafanikio ya vikosi vya Ukraine katika eneo la Kherson yanakuja baada ya miezi kadhaa ya operesheni ya kuvikabili vikosi vya Urusi kusini mashariki na mashariki ya nchi hiyo.

Vikosi vya Ukraine vinasema kuwa vilifanya oparesheni 'zilizofaulu' kwenye ukingo wa mashariki wa Dnipro.