Vikosi vya Uturuki vyashambulia waasi wa Kikurd
1 Desemba 2007Matangazo
Maafisa wa jeshi la Uturuki wamesema,wameingia kaskazini mwa Irak kushambulia kundi la waasi wa Kikurd wapatao kama 50 hadi 60.Siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan alisema kuwa baraza lake la mawaziri limetoa idhini kwa jeshi kuwashambulia wanamgambo wa chama cha Kikurd cha PKK.
Uturuki imeimarisha idadi ya wanajeshi wake hadi 100,000 katika sehemu za milimani karibu na mpaka wake na eneo la kaskazini mwa Irak.Majeshi hayo yamewekwa tayari kwa uwezekano wa kuwashambulia waasi wa Kikurd wanaojificha kaskazini mwa Irak. Hilo ni eneo wanakoishi Wairaki wengi wenye asili ya Kikurdi.