Vikosi vya Uturuki vyavuka mpaka.
18 Desemba 2007Ankara.
Vikosi vya jeshi la Uturuki vimevuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Iraq katika juhudi za kuwafurusha waasi wanaotaka kujitenga wa Kikurd. Kwa mujibu wa duru za jeshi la Uturuki, wanajeshi 300 wamekuwa wakiwafuatialia waasi wa PKK maili chache ndani ya eneo la Gali Rash, eneo la milima karibu na mpaka wa nchi hizo mbili. Hatua hiyo inakuja baada ya ndege za kijeshi za Uturuki kushambulia kwa mabomu vijiji kaskazini mwa Iraq mwishoni mwa juma. Maafisa wa Iraq wamesema kuwa kiasi raia mmoja ameuwawa katika mashambulizi na kudai kuwa hatua zozote za kijeshi hapo baadaye zinapaswa kuratibiwa na utawala wa mjini Baghdad. Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili nchini Iraq katika ziara ambayo haikutangazwa.