1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Vikosi ya serikali vyakabiliana na waasi Syria

5 Desemba 2024

Shirika la kufuatilia Haki za Binadamu nchini Syria limesema vikosi vya nchi hiyo vimekabiliana na waasi karibu na mji wa katikati wa Hama ili kujaribu kusitisha harakati za kusonga mbele kwa waasi hao.

https://p.dw.com/p/4nluo
Syria | Aleppo | 2024 | Hayat Tahrir al-Sham
Waasi wenye itikadi kali za kidini wakishika doria katika maeneo ya mashambani ya Aleppo Magharibi.Picha: Juma Mohammad/AP Photo/picture alliance

Shirika hilo lenye makao yake nchini Uingereza limesema kufikia jana jioni, wapiganaji hao wa makundi ya waasi walikuwa wameuzingira mji wa Hama kutoka pande tatu.

Kulingana na shirika hilo, mapigano makali yalitokea wakati wa usiku kati ya waasi na vikosi vya serikali, hasa katika eneo la Jabal Zayn al-Abidin, kaskazini mwa Hama.

Soma pia: Umoja wa Mataifa watoa wito wa kupunguza uhasama Syria 

Mkuu wa shirika hilo Rami Abdel Rahman, amethibitisha kuzuka kwa mapigano hayo.

Mji wa Hama ni muhimu kimkakati kwa jeshi la Syria na unatumika kama eneo salama la kuulinda mji mkuu wa Damascus.