Viongozi wa kiraia waachiwa huru Guinea
11 Mei 2023Viongozi watatu wa mashirika ya kiraia nchini Guinea waliokuwa wanazuiwa gerezani kwa miezi kadhaa wameachiliwa huru "bila masharti" jana Jumatano, saa chache baada ya watu saba kuripotiwa kuuawa wakati wa maandamano ya kushinikiza kuachiliwa kwao.
Viongozi hao watatu wa chama kinachoupinga utawala wa kijeshi cha National Front for the Defence of the Constitution, FNDC Ibrahima Diallo, Mamadou Billo Bah na Oumar Sylla waliachiliwa majira ya saa nne za usiku, hii ikiwa ni kulingana na meneja wa mawasiliano wa chama hicho Abdoulaye Oumou Sow.
Mmoja ya mawakili waliowawakilisha, Me Salifou Beavogui(BEVAGUI) amesema kwenye taarifa kwamba upande wa utetezi uliarifiwa tu juu ya ya kuachiwa kwa wateja wao bila ya masharti yoyote, huku akiishutumu mamlaka kwa namna ilivyoiendesha kesi dhidi ya viongozi hao.