Serikali ya mseto ya Ujerumani yaafikiana kuhusu bajeti
5 Julai 2024Matangazo
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la kijerumani la dpa,lililopata taarifa hizo kupitia vyanzo kadhaa vya serikali.
Viongozi hao pia wamefikia makubaliano ya awali kuhusu mpango wa bajeti utakaoimarisha ukuaji wa kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 0.5 mwaka ujao.
Hatua ya kufikiwa makubaliano imekuja baada ya wiki kadhaa za mazungumzo kati ya Kansela Olaf Scholz, Waziri wa Uchumi ambaye ni naibu Kansela, Robert Habeck na Waziri wa Fedha Christian Lindner.
Bunge la Ujerumani linatarajiwa kuijadili rasimu hiyo ya bajeti kuanzia katikati ya mwezi Septemba na inaweza kupitishwa mwezi Novemba au Desemba.