Viongozi wa Ulaya wapo nchini Tunisia kujadili uhamiaji
11 Juni 2023Viongozi wa Italia, Ubelgiji na wengine wa Umoja wa Ulaya wako nchini Tunisia kwa mazungumzo leo hii Jumapili. Lengo la mazungumzo hayo ni kutafuta njia muafaka za shughuli za uokoaji wa kimataifa na wakati huo huo nchi hizo zinaazimia kurejesha utulivu Tunisia, nchi ambayo ni chanzo kikubwa cha uhamiaji kuelekea barani Ulaya.
Soma pia: Tunisia yashtakiwa katika mahakama ya Haki ya Afrika
Rais wa Tunisia Saeed Kais amesema masharti yaliyowekewa nchi yake yatasababisha mgogoro wa kijamii ambapo amesema hatua hizo ni udikteta wa nchi za magharibi.
Hata hivyo watunisia wengi wamekata tamaa na wamechoshwa na utawala Kais hali ambayo imewasukuma wengi wao kuhatarisha Maisha yao kwa kufanya safari za hatari za kuvuka bahari ya Mediterania ili kutafuta maisha bora katika bara Ulaya.