1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Viongozi waandamizi wa Marekani na China wamezungumza

12 Mei 2023

Afisa mmoja wa serikali ya Marekani amesema Mshauri Mkuu wa Usalama wa Ikulu ya White House Jake Sullivan alifanya mkutano na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi mapema wiki hii mjini Vienna

https://p.dw.com/p/4RFUi
USA Jake Sullivan
Picha: Manuel Balce Ceneta/AP Photo/picture alliance

Kulingana na afisa huyo, Sullivan alimweleza Wang Yi kwamba utawala wa rais Joe Biden unataka kuupa kisogo mvutano kati ya Washington na Beijing ulioshuhudiwa baada ya Marekani kulidungua puto kubwa la China kwa madai ya kuwa chombo cha kijasusi. Afisa huyo amesema kwenye mazungumzo hayo, pande zote mbili zimekiri kuwa kisa hicho cha mwezi Februari kilikuwa cha "bahati mbaya" na zimekubaliana kusonga mbele kwa kurejesha mawasiliano ya kawaida baina yao. Mkutano kati ya Sullivan na Wang haukutangwaza na pande zote mbili, lakini Washington imesema majadiliano ya maafisa hao waandamizi yalikuwa ya kirafiki na yenye manufaa.