1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipindi sasa vinapatikana kwenye podcasts!

19 Aprili 2011

Learning by Ear, mradi wa vipindi vipya vya DW kwa ajili ya Afrika. Kupitia mfumo wa ‘podcasts’ utasikia mfululizo wa michezo ya redio na makala za siasa na jamii, masuala ya afya na Jamii, uchumi na mazingira na elimu!

https://p.dw.com/p/OrKS
Picha: DW

Siasa na Ushiriki

Learning by Ear - Political Education and Participation - Getting involved
Picha: gettyimages

Siasa sio serikali na bunge tu. Kushiriki katika siasa huanzia nyumbani! Kukubali kujihusisha na masuala ya kijamii katika eneo lako kunaweza kuleta mabadiliko. Waafrika wengi wanajiunga na juhudi za kutafuta Afrika iliyo bora. Pata ujuzi kupitia mada kama vile mashirika ya kiraia, uhamiaji na ushiriki katika siasa kupitia mfululizo wa makala na michezo ya redio.

 

Masuala ya Afya na Jamii

Learning by Ear - HIV/Aids - Preventing the plague
Picha: laif

Kiasi ya watu milioni mbili huambukizwa virusi vya Ukimwi kila mwaka Afrika. Ugonjwa wa Malaria huua kiasi ya watu milioni moja kila mwaka Afrika. Ni rahisi kujikinga na magonjwa yote mawili. Tunatoa ushauri kuhusu uzazi wa mpango na tunaeleza jinsi ya kuepuka mimba zisizotarajiwa pamoja na magonjwa ya kuambukiza ya zinaa. Vipindi vyetu vimeandaliwa kukuelimisha na kukuburudisha.

Uchumi na Mazingira

Learning by Ear - Economy
Picha: LAI F

Kama unataka kufahamu jinsi jamii inavyofanya kazi au utandawazi unavyoathiri Afrika basi usikose kusikiliza vipindi vyetu vya michezo ya redio kuhusu uchumi. Bara la Afrika huchangia kidogo sana katika mabadiliko ya hali ya hewa, lakini ndilo linaloathirika zaidi. Mradi wa Learning by Ear, Noa bongo jenga maisha yako, unapeleleza mahusiano kati ya watu na mazingira barani Afrika. Tunazungumzia kuhusu kuenea kwa jangwa, uharibifu wa misitu na uvuaji wa samaki kupita kiasi usiofuata utaratibu - tunaeleza matatizo na kutoa njia za kuyatatua.

 

 

Elimu na Jamii

Learning by Ear - Computer and the Internet - Closing the digital divide
Picha: CORBIS

Tunaelezea jinsi kompyuta na intaneti zinavyofanya kazi. Msaada kwa wale wote wenye nia ya kufanya kazi kwenye ulimwengu wa sayansi ya kompyuta. Katika vipindi vingine tunatoa habari kuhusu taaluma mbalimbali na mawasiliano kwa umma kupitia vyombo vya habari. Learning by Ear, Noa bongo jenga maisha yako, inampeleka msikilizaji katika safari ya maisha ya kila siku. Ulimwengu unaotuzunguka umejaa maajabu mengi sana, hakuna anayeyatambua. Na mwisho tunajifunza zaidi kuhusu historia ya bara la Afrika.

 

*Podcasts* Ni aina ya faili za sauti kwenye mtandao. Faili hizi unaweza kuziweka kwenye simu yako au vyombo vya muziki aina ya 'ipod' na MP3 na kuzisikiliza kwa muda wako.