1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Visiwa vya Canari. Wahamiaji haramu wafa maji.

2 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPi

Kiasi wahamiaji 28 ambao walitaka kuingia katika nchi za Ulaya kinyume na sheria kutoka mataifa ya Afrika magharibi wamekufa maji wakati wakijaribu kuingia katika visiwa vya Canary.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Morocco MAP, miili yao ilipatikana katika pwani ya magharibi ya eneo la Sahara baada ya boti walilokuwa wakisafiria na ambalo lilikuwa limejaa bila kiasi kuzama.

Wahamiaji wengine 49 walikamatwa wakati wakijificha katika eneo hilo. Watu wanaowasili katika kisiwa cha Hispania cha Canary imeongezeka katika miezi ya karibuni.

Karibu wahamiaji 13,000 kutoka Afrika wamejaribu kuingia katika kisiwa cha Hispania cha Canary mwaka huu pekee.