1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Griffiths: Vita vya Gaza ni "usaliti dhidi ya ubinaadamu"

6 Aprili 2024

Mkuu wa ofisi ya masuala ya kiutu kwenye Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amevitaja vita vilivyoongezeka vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza kuwa ni "usaliti dhidi ya ubinaadamu."

https://p.dw.com/p/4eVEY
Mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths
Mkuu wa ofisi ya masuala ya kiutu kwenye Umoja wa Mataifa Martin Griffiths asema vita vinavyoendelea Gaza ni "usaliti dhidi ya ubinaadamu"Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Kwenye taarifa yake katika mkesha wa kumbukumbu ya miezi sita ya vita hivyo, Griffiths anayeachia wadhifa huo mwezi Juni ametoa wito wa nia ya pamoja ya kuwepo na adhabu ya usaliti huo.

Mkuu huyo aidha amezungumzia ufikishwaji wa misaada unaoendelea kudhoofika katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya mabomu, ukosefu wa usalama na viuzuizi.

Amesema hayo wakati ujumbe wa Hamas unaoongozwa na naibu mkuu wa kundi hilo huko Gaza, Khalil Al-Hayya ukijiandaa kwenda Cairo kesho Jumapili kwa ajili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano, baada ya kualikwa na wapatanishi wa Misri.