1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Sudan vimesababisha njaa katika kambi ya Zamzam

2 Agosti 2024

Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha vita vinavyoendelea Sudan kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF vimesababisha ukosefu wa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam ya mji uliozingirwa wa El-Fasher.

https://p.dw.com/p/4j37c
Sudan El Fasher tatizo la wa maji
Wanawake na watoto wachanga katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam, karibu na mji wa El Fasher huko Darfur Kaskazini, Sudan.Picha: Mohamed Zakaria/REUTERS

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, kambi hiyo ilikumbwa na ukosefu wa chakula katika mwezi uliopita wa Julai. Afisa wa shirika la misaada ya kiutu la Plan International, Mohammed Qazilbash, amesema, kambi ya Zamzam iliyoko katika jimbo la Darfur Kaskazini, awali ilikuwa makao ya wakimbizi laki tatu ila kwa sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu nusu milioni katika kipindi cha wiki chache tu zilizopita, kutokana na mapigano yanayoendelea El-Fasher.