1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Syria vilisababisha vifo 3,700 mwaka wa 2021

22 Desemba 2021

Shirika la haki za binadamu nchini Syria, limesema machafuko nchini humo yalisababisha vifo vya watu 3,746 mwaka huu wa 2021 pekee. Idadi hiyo ni ya chini ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/44iAl
Syrien | Trauer und Zerstörung nach Luftangriff | TABLEAU
Picha: Muhammed Said/AA/picture alliance

Kulingana na takwimu ambazo zilikusanywa na shirika la Haki za binadamu la Syria lenye makao yake makuu Uingereza, watu 1,505 miongoni mwa watu hao waliouawa walikuwa raia na 360 walikuwa watoto.

Idadi hiyo ya vifo ndiyo ya chini zaidi kuwahi kurekodiwa katika vita hivyo vya muongo mmoja. Isitoshe ni takwimu zinazothibitisha hali ya kupungua kwa mauaji kutokana na mapigano. Mwaka uliopita watu 6,800 waliuawa, na mwaka wa 2019 watu 10,000 walipoteza maisha yao.

Israel yafanya shambulio katika bandari ya Syria

Shirika hilo la haki za binadamu lenye mafungamano na vyanzo katika majimbo mengine ya Syria, limesema watu 297 wameuawa mwaka huu kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini na vilevile kutokana na mabaki ya vilipuzi vingine katika maeneo tofauti tofauti.

Mashambulizi ya kuviziana?

Shirika linalofuatilia milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini lilisema mnamo mwezi Novemba kwamba milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini nchini Syria imeshinda visa kama hivyo vinavyotokea Afghanistan, na kwamba idadi kubwa ya vifo kutokana na milipuko hiyo imerekodiwa.

Vita vya Syria vilianza mwaka 2011. Baada ya ukandamizaji mkali wa serikali dhidi ya waandamanaji walioipinga serikali. Katika miaka miwili iliyopita hakujashuhudiwa mapigano makali.
Vita vya Syria vilianza mwaka 2011. Baada ya ukandamizaji mkali wa serikali dhidi ya waandamanaji walioipinga serikali. Katika miaka miwili iliyopita hakujashuhudiwa mapigano makali.Picha: Amer AlMohipany/NurPhoto/picture alliance

Hata hivyo, vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Urusi wakati mwingine hufanya mashambulizi katika ngome ya waasi Idlib iliyoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Licha ya hayo, makubaliano ya kusitisha vita yangali yanazingatiwa.

Kwa upande mwingine, wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS ambao walisitisha mashambulizi baada ya kundi lao kusambaratishwa mwaka 2019, pia wamekuwa wakifanya mashambulizi ya ghafla mashariki mwa Syria kisha wanatoweka.

Serikali, upinzani Syria kuandika katiba mpya

Urusi, Uturuki na Iran waongeza shinikizo dhidi ya Wakurdi

Hayo yakijiri, Urusi na Uturuki leo zimewashinikiza Wakurdi wa Syria kufanya mazungumzo na serikali ya Syria na waachane na malengo yao ya kujitenga.

Wito huo umejiri baada ya Urusi na Uturuki pamoja na Iran kujadili mustakabali wa Syria.

Tangu ushindi wa Rais Bashar al-Assad kwenye vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe, Kundi la Wakurdi limekuwa chini ya shinikizo kusalimisha silaha pamoja na jimbo wanalodhibiti la kaskazini mashariki.

Shirika linalofuatilia milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini lilisema mnamo mwezi Novemba kwamba milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini nchini Syria imeshinda visa kama hivyo vinavyotokea Afghanistan, na kwamba idadi kubwa ya vifo kutokana na milipuko hiyo imerekodiwa.
Shirika linalofuatilia milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini lilisema mnamo mwezi Novemba kwamba milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini nchini Syria imeshinda visa kama hivyo vinavyotokea Afghanistan, na kwamba idadi kubwa ya vifo kutokana na milipuko hiyo imerekodiwa.Picha: Hisam El Homsi/AA/picture alliance

Kwenye taarifa ya pamoja, baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Kazakhstan, Urusi, Uturuki na Iran zimesema zinaunga mkono mipaka ya Syria, zinapinga jaribio lolote la utengano na mipaka mipya na zina wasiwasi kufuatia shughuli za kundi linalotaka kujitenga mashariki mwa Mto Euphrates.

Putin, Assad wakutana Moscow

Baadhi ya viongozi wa Wakurdi wanataka uhuru kama suluhisho la mvutano lakini serikali ya Syria imelikataa pendekezo hilo.

Vita vya Syria vimesababisha vifo vya takriban watu nusu milioni na kuwa moja ya migogoro iliyosababisha idadi kubwa Zaidi ya watu kuwa wakimbizi au wahamiaji tangu kumalizika kwa Vita Vikuu Vya Pili.

Hadi leo, takriban watu milioni 2.8 hawana makazi kaskazini magharibi mwa Syria huku milioni 1.7 miongoni mwao wakiishi kwenye kambi au mahema wanayopewa na Umoja wa Mataifa.

(AFPE, RTRE, APE)