Haki za binadamuAfghanistan
Vizuizi dhidi ya wanawake vyazidi kuitenga Afghanistan
22 Juni 2024Matangazo
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMA Roza Otunbayeva amelimbia Baraza la Usalama kwamba vizuizi kwa wanawake na wasichana haswa katika elimu vimeendelea kuligharimu taifa hilo na kudhoofisha mustakabali wake.
Amesema vizuizi hivyo pia vinaondoa uaminifu juu ya uhalali wa vizuizi hivyo unaodaiwa na mamlaka ya nchini humo ya Taliban, ambao kulingana na afisa huyo inaendelea kuzuia suluhu za kidiplomasia zitakazoisaidia Afghanistan kuunganishwa tena kwenye jumuiya ya kimataifa.
Tangu waliporejea madarakani mwaka 2021, mamlaka ya Taliban haijatambuliwa rasmi na taifa lolote na imekuwa ikitumia sheria kali ya Uislamu, kukandamizwa uhuru wa wanawake unaotajwa na Umoja wa Mataifa kama "ubaguzi wa kijinsia."