1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Volodymyr Zelenskiy ashinikiza kupatiwa ndege za kivita

6 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema Poland itasaidia katika kuunda muungano wa mataifa ya Magharibi ili kuipatia nchi yake ndege za kivita wakati wanajeshi wake wakiendelea kutetea mji wa mashariki wa Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4PllQ
Poland, Warsaw, Volodomyr Zelensky | Olena Zelenska I Andrzej Duda
Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky akipokelewa na rais wa Poland Andrzej Duda Picha: Wojtek Radwanski/AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema Poland itasaidia katika kuunda muungano wa mataifa ya Magharibi ili kuipatia nchi yake ndege za kivita, wakati wanajeshi wake wakiendelea kutetea ngome yao ya mashariki ya Bakhmut dhidi ya mashambulio ya Urusi.

Zelensky amesema kuwa "hatutakiwi kusitisha mshikamano. Wakati vita vinahitaji silaha,mizinga na ndege za kivita, vinapaswa kutolewa bila kujali ni vipi Urusi italipokea hilo. Hivi ni vita vya kupigania uhuru, na haiwezekani kuvishinda nusu."

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewaambia mabalozi wapya wa Marekani na Umoja wa Ulaya kwamba nchi zao zinahusika kwa kiasi kikubwa na kuzorota kwa hali ya mahusiano yao tangu Urusi ilipotuma vikosi vyake nchini Ukraine mwaka jana.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, ameionya China kuwa, msaada wowote wenye hatari kwa Urusi katika vita vyake huko Ukraine, itakuwa kosa la kihistoria na lenye athari kubwa.