SiasaUfaransa
Von der leyen kukutana na Macron kabla ya ziara ya China
3 Aprili 2023Matangazo
Msemaji wa kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya Erid Mamer amesema viongozi hao wawili watajadiliana kuhusu masuala kadhaa ikiwemo vita vya Urusi nchini Ukraine,sekta ya nishati na maandalizi ya ziara yao ya China itakayojumuisha kuwa na mkutano wa pamoja na rais Xi Jinping.
Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Von der Leyen ametowa tathmini kuhusu sera ya China akisema kwamba nchi hiyo imeonesha kuongeza ukandamizaji nyumbani na kuonesha uthubutu zaidi nje ya nchi kwa kuondowa enzi ya mageuzi na kufungua milango na badala yake kuweka enzi ya usalama na udhibiti ambapo makampuni ya Kichina yanatakiwa kuisaidia serikali katika operesheni za ukusanyaji taarifa za kijaasusi.