VW yakataa mipango ya kupunguza gharama za uendeshaji
30 Novemba 2024Kampuni ya magari ya Volkswagen imekataa pendekezo la vyama vya wafanyakazi la kupunguza gharama katika shughuli zake nchini Ujerumani bila kufunga viwanda, jambo ambalo liliibua hasira kutoka kwa wawakilishi wa wafanyakazi huku migomo ikitarajiwa.
Kampuni hiyo imekuwa katika mazungumzo makali na chama cha wafanyakazi cha IG Metall tangu ilipotangaza mwezi Septemba mpango wa kufunga viwanda kadhaa nchini Ujerumani. IG Metall imeashiria kuwa mgomo unaweza kuanza Desemba 1 ikiwa VW haitasitisha mipango hiyo.
Soma pia: VW yaamuriwa kulipa fidia kashfa ya 'dieselgate'
Pendekezo la chama hicho lilijumuisha kufutwa kwa bonasi za usimamizi na wafanyakazi na kupunguza saa za kazi badala ya nyongeza ya mshahara. Hata hivyo, VW ilisema hatua hizo hazingesaidia kifedha kwa muda mrefu. Pande hizo mbili zinatarajiwa kuendelea na mazungumzo Desemba 9.