Vyama ndugu vya CDU/CSU vinapanga kumteuwa bibi Angela Merkel kushindana na kansela gerhard Schröder uchaguzi mkuu utakapoitishwa kabla ya wakati mwezi september ujao
24 Mei 2005Vyama ndugu vya Christian Democratic Union na Christian Social Union-CDU/CSU vinatazamiwa kumteuwa bibi Angela Merkel mapema wiki ijayoi kupigania kiti cha kansela uchaguzi mkuu utakapoitishwa miezi minne kutoka sasa.Madhamana wa ngazi ya juu wa CDU,waakiwemo mawaziri wakuu kadhaa wanamuunga mkonio bibi Merkel.Gazeti la mjini München „Münchener Merkur limemnukuu waziri mkuu wa wa Bavaria Edmund Stoiber akisema atafikiria uwezekano wa kuhamia Berlin baada ya uchaguzi mkuu ujao.Vyama vya Social Democratic SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne vimeshatangaza tangu jana majina ya watetezi wao.SPD wamemchagua kansela Gerhard Schröder na walinzi wa mazingira wamemchagua waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer kupigania wadhifa wa kansela.Chama cha Free Democratic FDP kitawakilishwa na kiongozi wake Guido Westerwelle.Kimeshaelezea haja ya kuunda serikali ya muungano pamoja na CDU/CSU mjini Berlin.