Vyama vya Pakistan vimekubaliana kuhusu muungano
14 Februari 2024Chama cha Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif na washirika wake wametangaza kuungana kwa pamoja na upinzani ili kuunda serikali ya mseto, na kumaliza hali ya sintofahamu iliyoibuka tangu wiki iliyopita, kufuatia kutokua na chama hata kimoja kilichopata wingi wa kura katika uchaguzi wa bunge uliofanyika kushindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja. Mazungumzo ya kufikia hatua hiyo yalihudhuriwa na kiongozi wa Pakistan People's Party aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Asif Ali Zardari na chama cha Sharif cha Pakistan Muslim League, akiwemo mdogo wake, Shehbaz Sharif, aliyechukua nafasi ya Khan alipoondolewa madarakani mwaka 2022. Akizungumza katika mkutano na wanahabari Shebaz hakusema kuwa ni nani atateuliwa katika wadhifa huo wa uwaziri mkuu, licha ya kuwa huenda kuna fununu kuwa Sharif angeongoza muhula mpya. Sharif amesemamazungumzojuu ya kuwa wataunda serikali ya muungano yalifanikiwa.