1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya serikali ya muungano Ujerumani kutatua mgogoro

5 Novemba 2024

Vyama vitatu katika serikali ya muungano ya Ujerumani vinaendelea na msururu wa mazungumzo ya kujaribu kupata mwafaka wa sera ya uchumi na mustakabali wa serikali hiyo ya muungano.

https://p.dw.com/p/4mekh
Ujerumani | Kansela Olaf Scholz
Kansela Olaf Scholz wa UjerumaniPicha: Hannes P. Albert/dpa/picture alliance

Muungano huo wa serikali ya Kansela Olaf Scholz unatarajiwa kukutana kesho kwa mkutano wake wa kwanza mkuu tangu mapumziko ya majira ya joto ya bunge, ila vyama hivyo vitatu vinatofautiana pakubwa katika sera ya uchumi.

Tofauti katika muungano huo zilianza kuonekana wazi baada ya waraka wa sera ya uchumi wa waziri wa fedha Christian Lindner,kuwekwa wazi Ijumaa iliyopita, ambapo alitaka sera nzima ya uchumi ya serikali ifanyiwe mabadiliko.

Soma pia:Ujerumani inaweza kukabiliwa na uchaguzi wa mapema

Tofauti zilizojitokeza kutokana na kuonekana kwa waraka huo zilipelekea uvumi wa uwezekano wa serikali hiyo kuvunjika na kutoa nafasi ya uchaguzi mpya kufanyika.

Kansela Olaf Scholz amesema leo kuwa ana imani kuwa mwafaka utapatikana. Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Robert Habeck, ametaka kuwepo na uvumilivu miongoni mwa wanachama akidai huu utakuwa wakati mbaya kwa serikali hiyo kuvunjika, ukizingatia kuna uchaguzi wa Marekani na vita vinavyoendelea vya Ukraine.