Vyombo vya habari na mustakabali wa lugha ya Kiswahili
2 Juni 2015Matangazo
Ingawa kuongezeka kwa vituo vya redio vinavyotumia lugha ya Kiswahili kwenye maeneo ya Afrika Mashariki kulitazamiwa kuwe neema kwa lugha hiyo, wasomi na wataalamu wa lugha wanahofia kwamba aina ya Kiswahili kinachotumiwa kwenye vituo hivyo vya redio kinakwamisha maendeleo halisi ya Kiswahili.
Mohammed Khelef alihudhuria Kongamano la 28 la Kiswahili lililofanyika katika mji wa kusini mwa Ujerumani, Bayreuth, na kuzungumza na Profesa Ken Walibora kutoka Kenya, ambaye kwanza anaelezea kiini cha wasiwasi alionao juu ya mustakabali wa lugha ya Kiswahili.
Kusikiliza mahojiano haya bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini
Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Josephat Charo