SiasaMexico
Waandamanaji Mexico wazuia mjadala majaji kupigiwa kura
11 Septemba 2024Matangazo
Picha za televisheni zimeonesha makundi ya waandamanaji wakiwa ndani ya ukumbi wa Seneti hali iliyomlazimisha rais wa baraza hilo la juu la kutunga sheria kuamuru vikao kusitishwa kwa muda usiojulikana.
Mpango huo wa Rais Andres Manuel Lopez Obrador, ambao wataalamu wanasema utaifanya Mexico kuwa nchi pekee duniani inayopiga kura kuwachagua majaji, umezusha maandamano makubwa ya umma, mtikisiko wa kidiplomasia na kuwatisha wawekezaji.
Rais Obrador ambaye anataka mpango huo upitishwe kabla hajakabidhi madaraka kwa rais mteule na mshirika wake wa muda mrefu Claudia Sheinbaum mnamo Oktoba, anasema mfumo wa sasa wa mahama unayaweka mbele maslahi ya wanasiasa na wafanyabiashara badala ya umma wa nchi hiyo.