"Mataifa ya Simba"
23 Januari 2013Ukuaji wa uchumi wa Afrika unaochochewa hususan na usafirishaji nje wa mali ghafi zake: madini kama vile shaba na nikeli, chuma cha pua na mawe ya thamani kama dhahabu na almasi, mafuta na gesi. Baadhi ya nchi kama vile taifa lenye kuzalisha mafuta la Angola yana ukuaji wake uchumi wa zaidi ya asilimia 20 kwa mwaka. Nchi nyengine zimeweza kufaidika kwa muda mfupi. Kwa mfano Msumbiji, nchi inayozungumza Kireno, iko kwenye mwelekeo mzuri wa kuzalisha kwa wingi kabisa makaa ya mawe na gesi duniani. Uchumi wa Afrika unanawiri wakati uchumi wa dunia ukizongwa na uhaba wa rasilmali.
Sambamba na neema hiyo ya malighafi, mfumo wa kiuchumi barani Afrika ni rahisi kuathirika kutokana na kutegema soko la dunia kuanzia bei hadi kuyumba kwa mahitaji. Uharibifu wa mazingira, rushwa au migogoro ya ugawanaji wa mali ghafi - yote hayo yana athari zake kwa utajiri huo mpya. Je, mkosi wa mali ghafi utaziharibu hatua muhimu za maendeleo zilizofikiwa? Kuna taathira gani ya neema ya mali ghafi kwa mataifa ya Afrika na watu wake? Waandishi wa DW wanatafuta majibu!